Picha Kwa Hisani –
Stivo Simple Boy ameibua hisia mseto mitandaoni baada ya kuchapisha picha akiwa ametulia na mrembo wa Kizungu.
Kwenye picha hiyo ya aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo anaonyeshwa akiwa ametulia na mrembo kifuani ambapo huenda alikuwa usingizini.
Stivo alichangamsha mitandao ya kijamii na picha hiyo aliyoiwekea ujumbe wa kitambulisho chake “ndio maanake” pamoja na emoji za mapenzi.
Huku baadhi ya wafuasi wake wakimpongeza mwimbaji huyo wa ‘Mapenzi Ya Pesa’ kwa kumtambulisha mrembo huyo, wengine walimuomba kuwa jasiri.