Picha kwa hisani –
Idara ya ulinzi nchini inaadhimisha siku ya wanajeshi wa KDF hii leo, ambapo sherehe za kitaifa za maadhimisho hayo zimeandaliwa katika kambi ya kijeshi ya Mariakani kaunti ya Kilifi.
Waziri wa ulinzi nchini Monica Juma tayari amewasili katika eneo hilo ili kuongoza sherehe hizo na anatarajiwa kutoa hotuba yake muda wowote kuanzia sasa.
Viongozi mbali mbali pwani wamehudhuria hafla hio akiwemo gavana wa Kilifi Amason Jeffa Kingi na sherehe za mwaka huu ni za tisa kuandaliwa.
Maadhimisho ya kwanza ya siku ya wanajeshi wa KDF ilifanyika mwaka 2011 baada ya kuzinduliwa oparesheni linda nchi,na kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni uimarishaji wa amani na usalama kupitia taasisi za kijeshi.