Picha kwa Hisani –
Kenya hii leo oktoba mosi imeungana na mataifa mengine yaliowanachama wa umoja wa mataifa kuadhimisha siku ya kimataifa ya wazee.
Mtaalam huru wa wazee katika baraza la umoja wa mataifa Rosa Kornfeld matte ametoa wito kwa kila mtu kusimama kidete kwa ajili ya kuhakikisha haki za wazee zinatimizwa.
Rosa ameongeza kuwa kukosekana kwa chombo maalum cha kisheria kwa ajili ya wazee ndiko kunakoeleza pia ukosefu wa kupewa kipaumbele kwa changamoto maalum zinazowakabili wazee.
Huku maadhimisho hayo ya siku ya wazee yakifanyika ,humu nchini kenya wazee wengi wametajwa kuishi katika umaskini kwa kukosa waangalizi,serikali ikihimizwa kujenga vituo maalum vya kuhifadhi wazee hao.