Picha kwa Hisani –
Siasa zinazoendelezwa kwenye swala la ugavi wa mapato katika Kaunti kwa kiwango kikubwa zimeathiri shughuli za kimaendeleo mashinani.
Kinara wa vuguvugu la ‘Mwamko mpya Pwani’ Bi Mirajj Abdillahi amesema siasa hizo hazifai na ni lazima bunge la Seneti kuwa wazi kuhusu suala hilo ili lisimuathiri mwananchi mashinani.
Kulingana na mwanaharakati huyo wa kisiasa na maendeleo Pwani, kiwango kilichofikia cha kuwatia nguvuni kiholela baadhi ya Maseneta ili kuwazuia kuchangia katika mjadala huo ni hatari.
Mirajj ametaka utata huo kutanzuliwa haraka iwezekanavyo na serikali za Kaunti kupata fedha za maendeleo kama inavyostahili.