Siasa za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msambweni zinazidi kushamiri huku wagombea mbalimbali wa kiti hicho wakizuru mashinani na kuwarai wakaazi kuwachagua.
Mgombea wa eneo bunge hilo kupitia chama cha Wiper Shee Abdulrahman akiwa katika kampeni zake za uchaguzi huo kule Kinondo katika eneo bunge hilo, ameahidi kuwasaidia wavuvi kuboresha shuhuli zao iwapo ataibuka mshindi.
Abdulrahman ameahidi kuwa kuwatafutia wavuvi wa eneo bunge la Msambweni leseni za uvuvi ili kuimarisha sekta hiyo sawia na kuanzisha soko la Samaki kama njia moja wapo ya kubuni ajira kwa wafanya biashara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitaifa chama cha Wiper Balozi Chirau Ali Mwakwere amewarai wakaazi wa Kinondo kumchagua Shee Abdulrahman kuwa mbunge wao huku akiwatahadharisha dhidi ya viongozi walaghai kuhusu swala la ajira.