Picha kwa hisani –
Mgombea wa urais wa zamani Peter Kenneth amepuuzilia mbali madai kuwa serikali imekuwa ikitumia mamlaka yake vibaya na kuwapiga vita wanasiasa wanaolenga kuwania nafasi za juu za serikali wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Akizungumza wakati wa ibada ya Misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la Kirwara, Kenneth amesema jinsi mwafaka ya kuepuka mvutano kati ya wanasiasa na serikali ni kuzingatia sheria za nchini.
Kenneth aliyekuwa ameandamana na Mbunge wa Gatanga Nduati Ngugi na Peter Kimari wa eneo bunge la Mathioya, Kenneth amesema ni lazima watu waliohusika katika uhalifu watiwe nguvuni licha ya kuwa ni wanasiasa huku akishikilia kuwa taifa hili linahitaji utulivu.
Kauli yake imejiri siku moja tu baada ya Naibu Rais Dkt William Ruto kudai kuwa makachero wa Idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI, wale wa Tume ya EACC na maafisa wa polisi kuhujumu mikutano yake ya kisiasa.