Picha kwa hisani –
Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amewasilisha maombi ya kutaka kupewa tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha ODM mbele ya Bodi ya kitaifa ya uchaguzi wa chama hicho.
Joho tayari amelipa ada zote zinazohitajika na bodi ya kitaifa ya chama hicho ikiwemo ada ya shilingi milioni moja huku bodi hiyo ikiongeza mda wa wale wanaotaka kuwasilisha maombi yao hadi tarehe 31 mwezi Machi.
Mwenyekiti wa kitaifa wa bodi hiyo Catherine Mumma, amesema bodi hiyo imeafikia uamuzi wa kuongeza mda zaidi kwani kuna baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaotaka pia kuwasilisha maombi yao.
Kulinagana na bodi ya chama hicho, mtu yeyote anayetaka kuwania urais kupitia chama hicho, ni lazima awe mzaliwa kwa Kenya, mpiga kuraaliyesajiliwa, Mwanachama wa kudumu, awe na shahada ya kutoka kikuu kinachotambulika nchini na pia awe na ripoti nzuri ya uadilifu na uwajibikaji.
Wakati huo uo, bodi hiyo ya uchaguzi ya chama cha ODM, imesisitiza kuwa ni lazama mtu huyo awe pia anastakabadhi zote hitajika kuwa kuwania kiti cha urais kwa mujibu wa Tume ya IEBC.