Picha kwa Hisani –
Waziri wa Elimu nchini Profesa George Magoha amesema shule za msingi na upili za umma nchini zina uwezo wa kuwasajili wanafunzi wote wanaosomea shule za kibinafsi kwa sasa.
Akizungumza hapo jana Magoha amesema kuna nafasi nyingi zilizowazi katika shule na umma na kwamba wazazi waliona wanafunzi katika shule za kibinafsi hasa zile ambazo zimefungwa hawapaswi kuwa na hofu.
Magoha aidha amesema wizara ya Elimu pamoja na wizara ya Afya nchini wanaendeleza mazungumzo ya jinsi ya kuzuia maambukizi katika taasisi za elimu nchini akisema kwa sasa mazingira ya shule sio salama kwa wanafunzi.
Wakati uo huo amewataka wananchi kuzingatia masharti ya kiafya katika kuwazika wapendwa wao, na wala sio kuendeleza tamaduni katika hafla za mazishi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.