Picha kwa hisani –
Shule mbali mbali za msingi na upili katika kaunti zote sita za pwani zimerejelea shughuli za masomo hii leo wakati huu ambapo maambukizi ya corona yameonekana kupungua.
Katika kaunti ya Kilifi, mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Barani eneo la Malindi Emmanuel Kitsao amesema wapitia changamoto kuzuia wanafunzi kutokaribiana ikizingatiwa kwamba shule hio ina uhaba wa madarasa sawa na kukosa maeneo yaliona kivuli kuendeleza masomo.
Kitsao amesema wanazingatia suala la wanafunzi kuvaa barakoa,kuosha mikono mara kwa mara sawa kuwapima viwango vya joto mwili ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo miongoni mwao.
Na katika kaunti ya Mombasa, kaimu mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Tononoka ambayo ni kati ya shule zilizoathirika na janga la corona Benjamin Nzaro,amesema wameeka mipangilio hitajika kuzuia maambukizi miongoni mwa walimu na wanafunzi.
Katika kaunti ya Taita taveta mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Voi Mumia Mvuria amesema watahakikisha wanafunzi wanaendeleza masomo kwa kuzingatia umbali wa mita moja na zaidi licha ya shule hio kukumbwa na uhaba wa madarasa.