Story by Mwanaamina & Mdune-
Shule ya msingi ya Masimbani iliyoko eneo la Kikoneni eneo bunge la Lungalunga kaunti ya Kwale imeorodhesha matokeo bora ya mtihani wa kitaifa wa KCPE ambapo mwanafunzi wa kwanza ni msichana na amepata alama 413.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo John Malinge Kanga amesema mwanafunzi wa pili katika shule hiyo amepata alama 411 na mwanafunzi watatu akipata alama 408.
Hata hivyo Mwalimu huyo mkuu amesema takribana wanafunzi 20 wamepata alama 400 katika shule hiyo na kuchangia shule hiyo ya msingi ya Masimbani kuorodhesha jumla ya alama 395.3
Katika Shule ya msingi ya kibinafsi ya Mumtaz iliyoko mjini Kwale, mwanafunzi wa kwanza katika shule hiyo ni Mwachughu Japhet Swaleh aliyepata alama 398, akifutwa na Mugaza Ndurya kwa alama 382 na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Khulud Faraj Karma aliyepata alama 373.
Na shule ya msingi ya Samburu katika eneo bunge la Kinango, mwanafunzi wa kwanza Joshua Patrick Mkalla amepata alama 403, Priscillah Chiboya akipata alama 374 na Joyce Medza Nyanje akipata 372.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mgunya Mganga amedai kurishidhwa na matokea hayo huku akiwataka wazazi kuchukua jukumu la kuwapa elimu watoto wao.
Hata hivyo Shule ya msingi ya kibinafsi ya Modern Green Hills eneo la Samburu imeoroidhesha matokeo bora kwani mwanafunzi wa kwanza Amina Sakina amepata alama 415, Mohammed Mwinyi alama 403, huku Christine Chizi akishilia nafasi ya tatu na 403.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Emmanuel Mwayaya amesema licha ya shule za eneo hilo kukumbwa na changamoto za ukame, wanafunzi wameorodhesha matokeo bora.
Wakati uo huo shule ya msingi ya kibinafsi ya Muungano eneo la Samburu imeorodhesha mwanafunzi bora Mariam Umazi Chiluku aliyepata alama 420, akifutwa na Blessing Uchi Mkamba kwa alama 416 na nafasi ya tatu akiwa Priscila Nadzua Kondo aliyepata alama 413.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Elias Ndonga amesema matokeo hayo yametokana na juhudi za walimu kwa ushirikiano na wazazi na wanafunzi.