Story by Hussein Mdune-
Kuna haja ya shule za kibinafsi nchini kufaidika na chakula cha msaada ambacho kinatolewa na serikali kuu
Haya ni kulingana na wadau wa maswala ya elimu kutoka eneo la Samburu wakiongozwa na Hamis Rai Nyondo, aliyesema licha ya chakula cha msaada kufika mashinani, shule nyingi za kibinafsi hazijafaidika na chakula hicho.
Rai ambaye ni mkurugenzi wa shule ya kibinafsi ya Muungano ilioko gatuzi dogo la Samburu amesema wakati huu ambapo mitihani ya kitaifa inatarajiwa kuanza kuna haja ya shule hizo pia kupewa chakula hicho ilikusaidia watahiniwa.
Hata hivyo amewataka wazazi ambao wanajimudu kushirikiana na uongozi wa shule ili kuona kwamba wanatoa chakula kwa watahiniwa wakati huo wa mitihani ya kitaifa.