Story by: Gabriel Mwaganjoni
Mbunge wa Kinango Gonzi Rai ameapa kuboresha hali ya miundo msingi katika shule mbalimbali eneo bunge hilo ili kuhakikisha Wanafunzi wanasoma katika mazingira yanayostahili.
Gonzi aliyezuru shule ya upili ya Wavulana ya Taru, ile ya Mgalani na Mwavumbo ili kukagua hali ya miundo msingi na viwango vya elimu katika shule hizo, amesema shule hizo zitaboreshwa kwa vifaa vya kutosha ili kuhakikisha wanafunzi hawataabiki pindi wanapoendelea na masomo yao.
Kulingana na Gonzi, atafanya kila juhudi ili kuimarisha viwango vya elimu katika eneo bunge lake.
Wakati uo huo, Mbunge huyo wa Kinango amewahimiza wanafunzi kujizatiti masomoni ili vwaweze kuliweka eneo bunge hilo kileleni katika nyanja ya masomo.