Story by Mwanamina Fakii –
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Ng’odzini katika eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale wamenufaika na ufadhili wa mabweni mawili kutoka kwa Shirika la linaloangazia ufadhili wa wanyamapori la Born Free na Serikali ya Japan.
Akizungumza katika halfa ya kupokeza rasmi mabweni hayo usimamizi wa shule hiyo Meneja wa Shirika la Born Free Tim Oloo amesema Shirika hilo limekuwa likitoa ufadhili kwa jamii ambazo zinapatana na mbuga za wanyama ili kujenga uwezo.
Kwa upande wake Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema hatua hiyo itaboresha viwango wa masomo shuleni humo.
Mvurya hata hivyo ameipongeza serikali ya Japan kwa ufadhili huo wa mabweni hayo mawili, akisema ujenzi wa mabeni hayo umegharimu takriban shilingi milioni 14.
Halfa hiyo pia imehudhuriwa na Balozi wa Japan humu nchini Horie Ryoich pamoja na wadau wengine wa sekta ya elimu kaunti ya Kwale.