Picha kwa hisani –
Wanafunzi zaidi ya 800 wa shule ya msingi ya Lukore gatuzi dogo la Matuga kaunti ya Kwale, huenda wakakosa mahali pa kujisaidia wakati shule zitakapofunguliwa mwakani kufuatia ukosefu wa vyoo vya kutosha.
Kulingana na Mwalimu wa shule hiyo Kuwania Mwakusema,idadi ya wanafunzi inahusisha wale wa msingi, chekechea na wenye uwezo maalum .
Mwakusema amesema vyoo vya shule hiyo viliporomoka miaka miwili iliyopita na kufikia sasa hawajajengewa vyoo vilivyo salama.
Hata hivyo amesema hali hiyo imeweka wanafunzi katika hatari ya kupata magonjwa kufuatia baadhi yao kutumia sehemu za wazi kwenda haja.
Kwa sasa usimamizi wa shule hiyo unaitaka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Kwale kusaidia katika ujenzi wa vyoo katika shule hiyo.