Mmoja wa wapiganiaji wa uhuru nchini Enock Ondego, ameitaka serikali kuwatambua mashujaa waliochangia upatikanaji wa uhuru nchini.
Katika mkao na meza ya muliko Ondego amesema kuwa serikali imewasahau wapiganiaji wa uhuru nchi, huku wengi wao wakiishi katika maisha ya uchochole.
Ondego amesimulia historia yake ambapo alipigwa na wakoloni kwenye harakati za kuitetea Kenya, hali iliyompelekea kupoteza uwezo wa kutembea miaka 57 iliyopita.
Amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuandaa kikao na mashujaa wote waliopigania ukombozi wa taifa hili, kama njia moja wapo ya kuwapongeza.
Taarifa na Michael Otieno.