Picha kwa Hisani –
Huku ujenzi wa daraja la kisasa la kufungwa na kufunguliwa ukiendela katika eneo la Likoni, ujenzi wa maeneo ya kuwawezesha wakaazi kupanda na kushuka daraja hilo vile vile umezinduliwa rasmi.
Mshirikishi mkuu wa utawala katika Ukanda wa Pwani John Elungata amesema ujenzi huo unaendelea katika pande zote za Kisiwani Mombasa kule Liwatoni na maeneo ya Likoni.
Akizungumza na Wanahabari mjini Mombasa, Elungata amesema ujenzi wa maeneo ya watu kutumia daraja hilo utawajumuisha vijana wa eneo la Likoni ili wapate ajira.
Kwa upande wake, Mhandisi wa kampuni iliopewa kandarasi ya kujenga daraja hilo, Mohamed Jalan amesema daraja hilo litakalogharimu shilingi bilioni 1.7 linatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.