Huenda Shughuli katika serikali ya kaunti ya Kilifi zikasambaratika kufuatia uhaba wa pesa unaokumba kaunti hiyo kwa sasa.
Akiongea na wanahabari huko Gede Spika wa Bunge la kaunti ya Kilifi Jimmy Kahindi amekiri kwamba hakuna mradi wowote unaoendelea kufikia sasa tangu kupitishwa kwa bajeti miezi miwili iliyopita.
Aidha Kahindi amefichua kuwa kati ya shilingi bilioni 13 ambazo serikali hiyo ya kaunti inahitajika kupokea kila mwaka, kufikia sasa ni shilingi milioni 500 pekee walizopokea ambazo hazitoshi.
Kahindi amedokeza kwamba bunge la kaunti ya Kilifi limelazimika kutafuta njia mbadala kutafuta fedha za miradi.
Taarifa na Charo Banda.