Picha kwa hisani –
Shughuli za kujadili maswala muhimu ya miradi ya maendeleo sasa zimeanza kusambaratika baada ya bunge la Kaunti ya kilifi kusitisha vikao kufuatia kisa cha maambukizi ya Corona kuripotiwa katika bunge hilo.
Akizungumza mjini Malindi mwakilishi wa wadi ya Gongoni katika eneo bunge la Magarini Kaunti ya Kilifi Albert Kiraga, ambaye pia ni mwenyekiti wa bajeti, amesema kuwa baadhi ya shughuli kama vile kupitishwa kwa miradi ya maendeleo ya pamoja na bajeti ya ziada ya mwaka wa kifedha wa 2020/2021 imeathirika pakubwa.
Kiraga amehoji kuwa kuna mikutano ambayo inapaswa kuandaliwa wakiwa pamoja kama kamati ya bajeti, na Wala sio kwa njia ya video kama wanavyostahili kufanya kwa kipindi hiki cha Corona.
Aidha Kiongozi huyo amesema kuwa kwa sasa hawawezi kwenda nyanjani kutathmini miradi inayotekelezwa na hata kuwasilisha malalamishi bungeni, kutokana na hali ilivyo kwa sasa.