Story by: Gabriel Mwaganjoni-
Shughuli za masomo zimekatizwa katika shule ya msingi ya Nyali eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa baada ya wazazi wa shule hiyo kuandamana wakipinga kuajiriwa kwa Naibu mwalimu mkuu mpya shuleni humo.
Wazazi hao wakiongozwa na Uzel Jean wamesema Omar Babu ambaye amekuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa kipindi cha miaka 20 sasa ameiongoza shule hiyo vyema na kusajili matokeo bora zaidi ya mtihani wa darasa la nane KCPE na hatua ya kuondolewa kwake ni makosa.
Wazazi hao wakishirikiana na watetezi wa haki za kibinadamu kutoka Shirka la MUHURI wameapa kumbandua afisini Kaimu mwalimu mkuu Toney Ogunga wakisema kuajiriwa kwake kumefanywa kinyume hasa ikizingatiwa kwamba tayari shule hiyo ya kijami iliyo na zaidi ya wanafunzi 1,000 ina manaibu walimu wakuu wawili.
Kwa upande wao wazazi wa shule hiyo Mohammed Mohammed na Ahmed Twahir wamesema shughuli za shule hiyo zinaendelezwa kiholela na bodi hiyo, huku Katibu wa Bodi Paul Munyao akifanya maamuzi bila ya kuwahusisha wazazi wa shule hiyo.
Wakati uo huo, Twahir amemsihi Rais William Ruto na Waziri wa Elimu nchini Ezekiel Machogu kuingilia kati mzozo huo ili kuinusuru shule hiyo ambayo inakabiliwa na uongozi duni na visa vya wizi wa fedha za wazazi.
Tayari Wazazi wa shule hiyo wameishtaki bodi ya shule kwa madai ya wizi wa shilingi milioni 6 fedha za shule hiyo, na sasa wameapa kuwasilisha kesi ya pili mahakamani kuhusu swala la uajiri