Picha kwa hisani
Mwenyekiti wa kamati ya afya katika baraza la magavana nchini Mohamed Kuti amesema iwapo shughuli za kiuchumi humu nchini zitafunguliwa hii leo ni lazima mikakati ya kuzuia maambukizi ya Corona iendelee kuidhinishwa.
Akizungumza na wanahabari Kuti ambaye pia ni gavana wa Isiolo amesema kwa sasa maambukizi ya Corona yanaongezeka kwa kasi na kwamba serikali kuu na zile za kaunti hazipaswi kulegeza kamba katika kuzuia maambukizi zaidi.
Kuti ambae pia ni gavana wa Isiolo ameshikilia kwamba serikali inapaswa kufungua shughuli za kiuchumi kwa awamu, kwa kuanza kwa kufungua sekta muhimu pekee.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya afya katika baraza la magavana amesema serikali kuu na serikali za kaunti wanawajibika kuzuia kusambaa kwa maradhi hayo,wananchi pia wanajukumu kubwa kuhakikisha ugonjwa huo hauenei zaidi.
Kauli yake imejiri wakati ambapo rais Uhuru Kenyatta adhuhuri ya leo anatarajiwa kuhutubia taifa kuhusu mikakati ya serikali ya kuzuia maambukizi ya corona nchini.