Shughuli ya kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msambweni, Wadi ya Wundanyi/Mbale na Dabaso kule kaunti ya Kilifi inaendelezwa kwa sasa.
Maafisa wa tume ya IEBC wameapa kuandaa uchaguzi huru na haki huku polisi wakiimarisha doria kuhakikisha uchaguzi huo unandaliwa vyema licha ya purukushani kushuhudiwa awali.