Mashabiki wa msanii kutoka label ya Wasafi wamekuwa na wasi wasi kuwa tamasha lake lisingefanyika baada ya mkahawa wa Bidi Badu kuchomoka.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Lavalava amewahakikishia mashabiki wake kuwa tamasha hilo litaendelea kama ilivyopangwa.
Kulingana naye sehemu iliyopatwa na mkasa inakarabatiwa kwa sasa na tamasha litaendelea kama ilivyopangwa siku ya Jumamosi.
Poleni Sana Ndugu Zangu Wa Bidibadu Kwa Hii Ajali Ya Moto Jamani Hili Ndilo Eneo Ninalotakiwa Kufanya Show Siku Ya Jumamosi Bidibadu Limeteketea Kwamoto Siku Ya Jana Lakini Kutokana Na shauku Kubwa Ya Mashabiki Na Maombi Yawengi Wameomba Eneo Lirekebishwe Haraka Iwezekanavyo Ili Juma Mosi Show Iwepo Kwahiyo Sasa Linarekebishwa Na Show Juma Mosi Itakuwepo Kama Kawa Tunakuja Kukiwasha #WCB4LIFE @bidibadu
Taarifa na Dominick Mwambui.