Picha kwa hisani –
Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu litawasilisha ripoti rasmi kuhusu dhuluma dhidi ya binadamu kwa umoja wa mataifa ya Afrika ili kutafuta haki za waliodhulumiwa.
Afisa wa maswala ya dharura katika shirika hilo Francis Auma amesema kwa mwaka mzima sasa Shirika hilo limekuwa likikusanya ripoti za ukiukaji wa haki za kibinadamu katika Kaunti zote sita za Ukanda wa Pwani.
Kulingana na Auma, Kaunti za Kwale, Mombasa, Kilifi na Lamu zimeangaziwa zaidi huku dhuluma zinazotokana na vita dhidi ya ugaidi na mauaji ya kiholela miongoni mwa Wakaazi wa Ukanda wa Pwani zikijitokeza kwa wingi.
Auma amesema kwa sasa Watetezi hao wa haki za kibinadamu wako mashinani katika Kaunti ya Lamu wakiangazia swala hilo la ukiukaji wa haki za kibinadamu na kuapa kutumia mbinu zote ili kukomesha hali hiyo.