Katika juhudi za kuendeleza mchakato wa uwiano wa kitaifa, sasa Shirika la kijamii la ONUG limezindua mpango maalum wa kuwaleta vijana pamoja ili kuwahamasisha dhidi ya athari za kujihusisha na vurugu.
Kulingana na Naibu Mwenyekiti wa Shirika hilo nchini Agnes Awuor, mara kama mara vijana wamekuwa wakihusika kwenye vurugu zinazotokana na uchochezi wa kisiasa hali ambayo imechangia taifa hili kukosa amani na kusalia nyuma kimaendeleo.
Akihutubu kwenye Kongamano lililowaleta pamoja vijana kutoka maeneo tofauti mjini Mombasa, Agnes amefichua kuwa kufuatia maridhiano kati Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga swala la uwiano miongoni mwa vijana linafaa kuangaziwa.
Kwa upande wake Mshirikishi wa Shirika hilo tawi la Mombasa Zakia Mohamed amewalaumu wazazi kwa kushindwa kuwalea watoto wao vyema kwa kuzingatia maadili, akisema hali hiyo ndio imechangia kushuhudiwa kwa vurugu za mara kwa mara.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.