Picha kwa hisani –
Shirika la reli nchini limeidhinisha safari za usiku za gari moshi za abiria kupitia reli ya kisasa ya SGR kuanzia leo usiku.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Philip Mainga safari za gari moshi hizo za abiria kutoka Mombasa kuelekea Nairobi na ile ya Nairobi kuelekea Mombasa itang’oa nanga rasmi mwendo wa saa tatu usiku hii leo.
Mainga amesema gari moshi hizo zitawasili maeneo husika mwendo wa saa tisa alfajiri hapo kesho,na kwamba kuidhinishwa kwa safari za usiku za gari moshi kuna lenga kurahisisha usafiri wa wanafunzi.
Mainga amesema safari hizo za usiku zitaendelezwa kwa siku mbili pekee kuanzia hii leo,na kwamba wataongeza muda wa safari hizo iwapo watabaini kuna idadi ya juu ya abiria.