Story by Gabriel Mwaganjoni
Utata umeikumba tena familia moja katika eneo la Mtwapa kaunti ya Kilifi kufuatia malumbano ya ni nani atakayeishi na mtoto wao wa miaka 3.
Mgogoro huo umefika katika Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la MUHURI na kuchangia Afisa wa maswala ya dharura katika shirika hilo Francis Auma kufika mahakamani kutafuta mwafaka kuhusiana na swala hilo.
Auma amesema Mamake mtoto huyo Hellen Maria ambaye alizaa na raia mmoja wa Uingereza Kevin Burry kwa sasa hajui mwanawe aliko na amekuwa akihangaika kimawazo.
Kwa upande wake Maria aliyekuwa akizungumza nje ya majengo ya mahakama ya Mombasa alipopata kibali cha kuishi na mwanawe siku 4 huku Burry akiruhusiwa na mahakama kuishi na mwanawe siku tatu ndani ya juma moja amesema mahakama imemhangaisha mno.