Kufuatia msongo wa mawazo miongoni mwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa uliochangiwa na janga la Corona, Shirika la Msalaba mwekundu limewekeza katika kutoa ushauri nasaha kwa waathiriwa.
Mshirikishi mkuu wa shirika hilo tawi la Mombasa Mohammed Rajab amesema juhudi hizo zinatokana na idadi kubwa ya waliopata maambukizi ya corona kuingiwa na hofu, huku wengine wakipoteza ajira.
Akizungumza mjini Mombasa,hapo jana Rajab amesema Shirika hilo limejizatiti kuhakikisha waathiriwa wanapewa mwelekeo, ili kuweza kuyakusanya upya maisha yao.
Kulingana na Rajab, watu wengi walinufaika na misaada ya kibinadamu kutoka kwa shirika hilo, japo misaada hiyo haikuweza kukimu kila mkaazi wa kaunti hiyo.