Shirika la maenedelo ya wanawake nchini limejitokeza na kueleza wasi wasi wake kufuatia ongezeko la dhulma za kingono,mauji na mimba za mapema miongoni mwa watoto nchini.
Katika kikao na wanahabari mwenyekiti wa kitaifa wa shirika hilo Bi Rahab Muiu amesema watoto wameathirika zaidi na janga la corona kwani wanapitia dhulma nyingi katika kipindi hiki.
Bi Rahab amesema umaskini miongoni mwa wanajamii umechangia watoto wengi kujihusisha na ngono za mapema,hali inayowaeka katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo maambukizi ya ukimwi.
Amezitaka serikali kuu na zile za kaunti kuongeza vyuo vya kiufundi ili kuhakikisha watoto wanaojifungua mapema na hasa wale wanaotoka familia maskini wanapata ujuzi wa kazi za mikono waweze kujikimu.