Story by Hussein Mdune-
Shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS limeanzisha mpango wa usambazaji maji katika vidimbwi vya maji kwenye misitu ya kaunti ya Lamu ili kuwasaidia wanyamapori kwa maji.
Afisa mkuu wa Shirika hilo kaunti ya Lamu Mathias Mwavita amesema hatua hiyo itazuia mizozo ya wanyamapori na binadamu katika kaunti hiyo kwani wanyama kama vile Viboko na Nyati wameonekana wakiwaangaisha wakaazi.
Mwavita amesema kufikia sasa zaidi ya Nyati 20 na viboko watatu wamefariki kutokana na ukame uliokithiri katika misitu ya kaunti ya Lamu.
Wakati uo huo amedokeza kwamba maeneo yalioathirika zaidi na ukame na kushuhudia visa vya mizozo ya wanyamapori na binadamu ni eneo la Bargoni, Hindi, Magogoni, Pandanguo, Witu, Dide Waride na baadhi ya maeneo ya Mpeketoni.