Story by Salim Mwakazi-
Kenya imejiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya bahari duniani huku Shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS likipokea vifaa vya kulinda mazingira ya baharini ikiwemo dau kutoka kwa Shirika la kimataifa la kuhifadhi mazingira la World Wide Fund for Nature -WWF.
Akizungumza katika eneo la Kisite/Mpunguti, Naibu mkurugenzi wa Shirika la KWS nchini Samuel Tokore amesema vifaa hivyo vitawasaidia maafisa hao kuwalinda wanyama wa baharini.
Tokore amesema vifaa hivyo vitawasaidia pia katika kufanya utafiti wa bahari sawa na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shirika la World Wide Fund for Nature Mohamed Awer amesema licha ya bahari ya Kenya kuwa katika hali nzuri bado kuna changamoto katika kuhifadhi mazingira ya bahari.