Shirika la Kilimo tawi la kaunti ya Mombasa linaomboleza kifo cha Meneja wa tawi hilo Peter Muema Mutisya aliyeaga dunia mjini Mombasa baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Mutisya alishinikiza mabadiliko katika Shirika hilo, hali iliyopelekea majengo ya Shirika hilo la ‘Agricultural Society of Kenya (ASK) tawi la Mombasa kukodishiwa Wafanyibishara, huku Wakulima wakiendelea kufunzwa kuhusu kilimo cha kisasa.
Mutisya vile vile alikuwa ameidhinisha mchakato wa kuwafunza wavuvi mikakati mbalimbali ya uvuvi na mpango wa Serikali wa uchumi wa baharini yaani ‘Blue Economy’ hali iliyopelekea ushirikano wa Shirika hilo na Serikali ya Mombasa.
Mwenyekiti wa Shirika hilo la kilimo tawi la kaunti ya Mombasa Bi Anisa Abdallah amemuomboleza Mutisya akisema maono yake ya kuimarisha shughuli za kilimo biashara yatatekelezwa na Shirika hilo kikamilifu.