Story by Ali Chete-
Shirika la kijamii la KECOSCE limeanzisha mchakato wa kuihamasisha jamii kuhusu ustahimilivu wakati huu ambapo taifa linashuhudia mihemeko ya kisiasa.
Afisa wa miradi katika shirika hilo Kibwana Hassan amesema kwa sasa taifa linashuhudia joto la kisiasa na hali hiyo huenda ikasababisha vurugu iwapo jamii haitahamasishwa kuhusu athari za mihemeko ya kisiasa.
Kibwana amesema tayari wamewapa mafunzo wanajamii katika kaunti zote sita za ukanda wa Pwani ambao watasambaza ujumbe wa amani hadi mashinani.
Kwa upande wake Afisa wa maswala ya nyanjani wa shirika hilo Mwalimu Rama amesema njia pekee ya jamii kuwa na amani ni kuhamasishwa ili kuwaepuka viongozi ambao watawachochea.