Story by Bakari Ali –
Shirika la kijamii la KECOSCE linaendeleza vikao vya hamasa kwa viongozi mbalimbali katika jamii kuhusu jinsi wanavyoweza kudhibiti mizozo mbalimbali.
Afisa wa maswala ya nyanjani katika Shirika hilo Mwalimu Rama amesema kutokana na kushuhudiwa joto la kisiasa nchini kuna haja ya mikakati muafaka kuidhinishwa ili kuzuia kutokea kwa ghasia wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Kwa upande wake, Kasisi Jonathan Dena amesisitiza haja ya kushirikishwa kwa vijana katika vikao hivyo vya hamasa kwani mara nyingi vijana wamekuwa wakitumia visivyo.
Wakati uo huo Kasisi Dena ameitaka serikali kutumia mbinu mbadala katika kutatua matatizo yanayolikumba taifa hili na wala sio kutumia nguvu au silaha kutafuta suluhu.