Story by Salim Mwakazi:
Shirika la kijamii la KECOSCE limeitaka serikali ya kitaifa kuwahamasisha wazee wa nyumba kumi katika maeneo ya mashinani ili kuimarisha usalama katika jamii.
Afisa wa Nyanjani wa Shirika hilo, Mwalimu Rama amesema hamasa hizo zitawawezesha wazee wa nyumba kumi kufahamu na kutelekeza majukumu yao ipasavyo.
Akizungumza katika kikao cha kuihamasisha umma kuhusu maswala ya amani na usalama katika eneo la Kombani kaunti ya Kwale, Rama amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha juhudi za serikali za kudumisha amani na usalama.
Kwa upande wake Katibu wa Baraza la mashauri ya kiislamu nchini KEMNAC tawi la kaunti ya Kwale Sheikh Amani Mwachirumu amependekeza kujumuishwa kwa wazee wa nyumba kumi katika mradi wa viongozi wa kidiniwa kuhubiri amani katika jamii.