Story by Janet Shume-
Shirika la kutetea haki za kibinadamu la HURIA limeipongeza idara ya polisi nchini kwa kuimarisha usalama wakati wa uchaguzi wa Agosti 9 katika eneo la Pwani.
Afisa wa Shirika hilo kaunti ya Kwale Mwinyihaji Chamosi amesema hakuna visa vyovyote vya ukiukaji wa haki za kibinadamu vilivyoripotiwa kwamba vilitekelezwa na maafisa wa polisi wakati wa uchaguzi huo.
Chamosi amedokeza kwamba ripoti ya uchunguzi iliyofanywa katika kaunti tatu za Pwani imeonyesha wazi kwamba maafisa wa polisi walitekeleza majukumu yao kwa kuambatana na sheria.
Wakati uo huo, amezidi kuwarai wananchi kudumisha amani wakati huu ambapo Viongozi wa Muungano wa Azimio wanawasilisha kesi Mahakamani ya kupinga uchaguzi wa rais mteule Dkt William Ruto.