Story by Mwanaamina Fakii-
Shirika la kutetea haki za kibinadamu la HURIA, limeeleza haja ya wanawake kuhusishwa kikamilifu katika hamasa zinazoendelezwa dhidi ya itikadi kali na ugaidi.
Afisa wa mipango katika shirika hilo Betty Sidi, amesema kwa sasa wanawake wanasajiliwa kwa wingi katika makundi ya itikadi kali na ugaidi na pia wanaongoza katika kuwashawishi watu wengine kujiunga katika makundi hayo.
Betty amehoji kwamba iwapo hakutaidhinishwa mipangilio ya kuzuia wanawake dhidi ya kusajiliwa katika makundi hayo, basi kizazi kijacho cha wanawake kitaangamia.
Wakati uo huo amesema wazazi wa kike ni kiungo muhimu katika mapambano yanayoendelea dhidi ya itikadi kali na ugaidi, kwani hutambua mapema mabadiliko ya tabia ya wanafamilia waliosajiliwa katika makundi hayo.