Story by Our Corresponents –
Idara ya Maji, Misitu, Mazingira, mali asili na usafi wa miji katika kaunti ya Kilifi inapania kuanzisha tena mradi wa kubadilisha maji taka kuwa gesi.
Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya usambazaji maji mjini Malindi MAWASCO Anderson Furaha, amesema mradi huo ambao ulikuwa umeanzishwa hapo awali na kisha kuharibiwa na mafuriko utaanzishwa tena hivi karibuni.
Furaha hata hivyo amedokeza kwamba kituo kitakachojengwa katika eneo la Sabaki kitakuwa kikubwa zaidi ili kuboresha mazingira kwa kubadilisha maji taka kuwa gesi.
Mwenyekiti huyo amesema tayari kampuni hiyo imepokea takribani shilingi milioni 120 ili kufanikisha mradi huo kutoka kwa Shirika la Water Sanitation Trust Fund.