Story by Our Correspondents –
Mwenyekiti wa Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC Askofu mkuu mstaafu Eliud Wabukala amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Tume hiyo imefanikiwa kurudisha shilingi bilioni 25 zilizokuwa zimeporwa.
Askofu Wabukala amesema fedha hizo zimetokana na kesi 169 za ufisadi zilizowasilishwa Mahakamani na mali za watu hao kuchukuliwa kutokana na ushahidi uliyoonyesha wazi kwamba fedha hizo zilikuwa zimeporwa kwa serikali.
Katika kikao na Wanahabari jijini Nairobi, Askofu Wabukala amesema Tume ya EACC imesaidia kuzuia wizi wa shilingi bilioni 34 zilizokuwa zimepangwa kuporwa na baadhi ya wakenya huku akisema maswala mengi ambayo tume hiyo imesaidia wakenya.
Kwa upande wake Jaji mkuu nchini Martha Koome amesema ufisadi umekuwa changamoto kubwa zaidi kuukabili hasa katika taasisi za umma na sekta za kibinafsi huku akisisitiza haja ya ushirikiano kati ya taasisi zilizo na ujuzi katika maswala ya kupambana na ufisadi nchini.