Picha kwa hisani –
Hueda ugatuzi kote nchini ukaboreshwa hata zaidi baada ya sheria kupitishwa inayolenga kuidhinishwa kwa afisi za mawakili, katika serikali za kaunti ya the County Attorneys.
Mshirikishi wa chama cha Mawakili eneo la Pwani Riziki Emukule, anasema hatua hiyo inalenga kutathimini ubora wa sheria zinazotungwa katika serikali hizo za kaunti.
Emukule pia anasema hatua hiyo itarahisisha utekelezaji wa miradi na sheria katika utekelezaji wa maendeleo mashinani kinyume na ilivyo sasa.
Wakati huo huo, ameipongeza hatua hiyo akisema itabuni nafasi zaidi za ajira katika taaluma ya uwakili.
Amezihimiza kaunti zote nchini kuhakikisha zinatekeleza sheria hiyo ili kurahisisha utendaji kazi.