Sherehe za harusi za usiku katika kaunti ya Kwale zimepigwa marufuku.
Kamishna wa kaunti hiyo Karuku Ngumo ametoa onyo kwa wakaazi wa kukoma kuandaa sherehe za usiku akisema kuwa zinasheheni maovu.
Ngumo amezitaja sherehe hizo ikiwemo harusi na Disco matanga kama chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama na zinazopelekea vijana kuporomoka kimaadili.
Ngumo amewahimiza machifu kuwa chonjo kuhakikisha sheria hio inatekelezwa kama njia mojawapo ya kuboresha usalama hususan nyakati za usiku.
Sikiliza hapa.
Taarifa na Salim Mwakazi.