Kutokana na sintofahamu ambayo inaendelea miongoni mwa wazee wa kaya wa Magarini na wale wa Malindi dhidi ya sherehe za Mekatilili sasa ni wazi kwamba sherehe hizo huenda zikasambaratika.
Kulingana na Katoi wa Tabaka ambaye ni mmoja wa waandalizi wa sherehe hizo ni kwamba hawajapokea ufadhili kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kilifi hali ambayo huenda ikafanya tamasha hiyo kukosa kufana.
Kulingana na Katoi ukosefu wa ufadhili huo umekuwa changamoto kubwa katika matayarisho ya sherehe hizo.
Kulingana naye walitarajia kutumia kima shillingi milioni 6 lakini kufikia sasa wamepata kias kichache mno.
Kwa upande wake afisa mkuu wa utamaduni katika serikali ya kaunti ya Kilifi Mwenda Karisa amesema kuwa serikali ya kaunti ya kilifi haiwezi kivyovyote vile kufadhili sherehe yote na kushikilia kwamba sherehe hizo niza kitamaduni zinazofaa kusimamiwa na miungano ya kaya na wala sio kaunti ya Kilifi pekee.