Picha kwa hisani –
Baraza la Mashauri ya Kiislamu nchini KEMNAC limetaka kutiwa nguvuni kwa Viongozi wa kidini wanaokiuka masharti ya kudhibiti maambukizi ya Corona katika nyumba za ibada.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Sheikh Juma Ngao amesema viongozi hao wanahatarisha maisha ya waumini na jamii vile vile, akipendekeza hatua kali za kisheria kuchukiliwa dhidi yao.
Wakati uo huo, Kiongozi huyo wa kidini amewakosoa vikali baadhi ya wakaazi hasa wa kaunti ya Mombasa ambao wanapuuzilia mbali mbinu za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Wakati uo huo amewataka wananchi kuhakikisha wanazingatia masharti yote ya kujikinga na Corona ili kuhakikisha virusi hivyo vinadhibitiwa.