Story by Gabriel Mwaganjoni –
Baraza la Mashauri ya Kiislamu nchini KEMNAC limeitaka Tume ya huduma za mahakama nchini JSC kutangaza wazi nafasi ya Kadhi mkuu nchini baada ya kukamilika kwa muhula wa Kadhi mkuu wa sasa Sheikh Shariff Ahmed Muhdhar.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Sheikh Juma Ngao amesema ni sharti Tume hiyo itangaze wazi jinsi ilivyotangaza nafasi za majaji na mkuu wa Sheria, akisema usajili huo haupaswi kufanywa kisiri.
Akiwahutubia waandishi wa habari katika kaunti ya Mombasa, Sheikh Ngao amesema ni sharti swala hilo lizingatiwe akidokeza kuwa baraza hilo limeiandikia barua tume hiyo kuwekwa wazi nafasi hiyo.
Wakati uo huo, Sheikh Ngao amehoji kwamba ni sharti wadhfa huo ukabidhiwe msomi na kiongozi aliye na tajriba ya hali ya juu.