Huku zikiwa zimesalia siku 11 uchaguzi mdogo wa msambweni kuandaliwa, Mgombea wa kiti Cha ubunge wa msambweni Shee Mahmoud Abdulrahman ameahidi kuboresha swala la afya kwa wakaazi wa msambweni.
Akiongea na wakaazi wa msambweni, Mahmoud amesema kuwa swala la afya lingali bado ni duni, na endapo atanyakua kiti hicho basi atahakikikisha swala hilo limetimizwa.
Aidha Amesema atawezesha kuzalisha ajira kwenye sekta ya uvuvi, kwani Amesema kuwa wengi wametegemea uvuvi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama Cha wiper nchini Balozi Ali Chirao Mwakwere ameunga mkono hatua hiyo huku akiwataka viongozi wanaogombea kiti hicho, kujitenga na siasa za kugawanya wananchi.
Wakati uo huo Amewataka wakaazi wa msambweni kutohadaiwa na kupotezwa kisiasa huku akiwarai kumpigia kura Shee Mahmoud Abdulrahman.