Picha kwa hisani –
Mgombea huru wa kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa eneo la Msambweni kaunti ya Kwale Mariam Sharlet Akinyi amejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Akizungumza katika eneo la Ukunda Sharlet amesema kwa sasa atamuunga mkono mgombea wa kiti hicho wa chama cha ODM Omar Boga baada ya kufanya mashauriano ya kina na kinara wa ODM Raila Odinga.
Sharlet amesema kujiondoa kwake kwenye kinyanganyoro hicho sio udhaifu na kwamba ana imani iwapo atashirikiana na Boga kwa pamoja watafanikisha masuala muhimu ya maendeleo kwa wakaazi wa Msambweni.
Kwa upande wao wanachama wa ODM wakiongozwa na mjumbe mteule katika bunge la kaunti ya Kwale Hanifa Mwajirani wameahidi kushirikiana na Sharlet wakisema kwamba wanaimani ODM itaibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo wa disemba 15.
Sharlet alijiondoa kwenye chama cha ODM na kuonyesha nia ya kujiunga na jubilee kabla ya kuwa mgombea huru wa kiti hicho baada ya Jubilee kutangaza kwamba haitaidhinisha mgombea kwenye uchaguzi huo.