Story by Gabriel Mwaganjoni –
Wahudumu wa Bodaboda katika kaunti ya Mombasa wamehimizwa kujitenga na malumbano ya wanasiasa yanayolenga kuwachochea na kuzua vurugu au kuharibu makongamano ya wanasiasa.
Akiwahutubia Wanabodaboda katika uwanja wa Tononoka kaunti ya Mombasa wakati wa uzinduzi wa chama cha wahudumu hao nchini, Mwanasiasa Suleiman Shahbal aliyechangia chama hicho shilingi nusu milioni, amewataka wahudumu hao kushiriki siasa za maendeleo na wala sio kugawanywa na wanasiasa.
Shahbal amesema mgawanyiko wa kisiasa kwa wahudumu hao una athari kubwa jamii nzima inayowategemea wahudumu hasa katika sekta ya uchukuzi wa umma.
Wakati uo huo, Mgombea huyo wa ugavana kaunti ya Mombasa katika uchaguzi mkuu ujao, amehimiza umoja wa wahudumu hao wa bodaboda ili wafaulu kiuchumi.