Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mfanyabiashara na Mwanasiasa Suleiman Shahbal ameweka wazi kwamba alifanya mashauri ya kina na Kinara wa Muungano wa Azimio la umoja One Kenya Raila Odinga kabla ya kuchukua uamuzi wa kujiondoa katika kinyang’anyiro cha ugavana wa kaunti ya Mombasa.
Shahbal aliyekuwa akiuhutubia umma katika sherehe za Eid Baraza zilizofanyika katika bustani la Treasury mjini Mombasa amesema maafikiano walioyafanya na Odinga yanalenga kuimarisha maswala ya uchumi wa ukanda wa Pwani.
Kulingana na Shahbal muaniaji wa ugavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir ana uwezo mkubwa wa kuleta mabadilko ya kimsingi katika kaunti hiyo.
Hata hivyo amemtaka Nassir na Viongozi wengine watakaoingia uongozini kuliwajibikia kikamilifu swala la maendeleo mashinani.