Story by Ali Chete-
Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal ameukosoa uongozi ulioko mamlakani kwa madai ya kushindwa kubuni nafasi za ajira kwa wakaazi wa Mombasa.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuapisha viongozi wa wahudumu wa tuktuk, Mwansiasa huyo ambaye pia ni Mwekezaji amesema uongozi uliopo sasa umefeli kuwasaidia vijana kiujiendeleza kimaisha.
Shahbal ameahidi kutoa malipo yanayolipishwa wahudumu wa tuktuk katika kaunti hiyo ili kuhakikisha wanajiendeleza na kukuza uchumi wa kaunti hiyo.
Wakati uo huo amedai kwamba yuko tayari kushirikiana na wakaazi wa kaunti ya Mombasa ili kuhakikisha wanasaidiana kuboresha maisha ya wakaazi sawa na kuwahimiza kumuunga mkono katika azma yake ya kuwania kiti cha ugavana wa kaunti hiyo.