Huduma za uchukuzi kupitia kwa barabara ya reli ya kisasa maarufu SGR zimepelekea manufaa makubwa katika sekta ya utalii Pwani.
Meneja wa hoteli ya kifahari ya Travellers eneo la Bamburi Kaunti ya Mombasa Fred Kiuru amesema kwamba shughuli za kibiashara zimeimarika pakubwa katika sekta ya mahoteli Kaunti hiyo kutokana na uchukuzi huo wa SGR.
Wakati uo huo Kiuru ametaja kuimarika kwa hali ya miundo msingi kama kulikochangia kuimarika kwa sekta ya kitalii huku watalii wa kinyumbani wakifurika Pwani ili kusherehekea Pasaka.
Wakati uo huo, baadhi ya wageni waliyozuru Pwani ili kujivinjari wamedhidhirisha furaha kufuatia mandhari bora katika mahoteli na maeneo mengine ya kujivinjari.
Kwa sasa, sekta ya mahoteli inashuhudia asilimia 100 ya wageni huku asilimia 90 wakiwa wageni wa kinyumbani na asilimia 10 wa mataifa ya nje yakiwemo Uingereza, Marekani, Utaliano, Ujerumani, Ubelgiji miongoni mwa mataifa mengine ya nje.