Story by Ephie Harusi–
Taasisi inayoangazia fedha za umma nchini IPF imeitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kuhakikisha kuna uwazi wanapofanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma katika idara mbali mbali za kaunti hiyo.
Afisa wa miradi katika taasisi hiyo Asha Kudura Bakari amesema ripoti ya hivi punde iliyotolewa na shirika hilo kwa ushirikiano na shirika la Internation Budget Partnership imebaini kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi imeshuka hadi asilimia 9 kutoka asilimia 30 katika kutimiza uwazi wakati wa ukaguzi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti hiyo kwa wadau mbali mbali mjini Kilifi Asha amesema hali hiyo imetokana na kutowajibika kwa viongozi.
Kauli yake imeungwa mkono na Jacob Acholla ambaye ni afisa wa ukaguzi wa miradi katika shirika hilo aliyesema ili kutimiza uwazi wakati wa ukaguzi serikali ya kaunti ya Kilifi inafaa kuwa na viongozi walio na uwazi.